Familia yetu iliumia, ilihuzunika sana na suala la Vanessa Mdee na madawa – Mimi Mars
Kama ambavyo ingetarajiwa kwa familia yoyote, familia ya Vanessa Mdee, ilihuzunishwa na tuhuma dhidi yake kuhusiana na dawa za kulevya.
Vee alitajwa kwenye orodha ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, na tangu mwishoni mwa wiki iliyopita alikuwa ameshikiliwa na polisi jijini humo kwa mahojiano kabla ya kuachiwa kwa dhamana, Jumatatu hii.
“Kusema ukweli kwenye hili suala la Vanessa na madawa, familia yetu tumehuzunika, tumeumizwa kwasababu tunajua ni mtu ambaye hawezi kufanya kitu kama hicho wala hawezi kujihusisha na vitu kama hivyo,” Mimi Mars ambaye ni mdogo wake na Vanessa, aliiambia tovuti ya MillardAyo.
“Lakini imetokea ametajwa inabidi tufuate sheria, tutafanyaje, lakini kusema ukweli tumeumizwa. Kizuri kinachotupa amani tunajua hawezi kufanya kitu kama hicho wala hawezi kujihusisha na mambo kama hayo,” aliongeza Mars.
Mimi Mars amedai kuwa ilimchukua muda kuja kupata taarifa kuwa dada yake naye ametajwa kwenye list ya Makonda hadi kaka yake alipompigia simu kumwambia.
“Kusema kweli hata sikumtumia message, for what? Sababu Najua there is no way, yaani hicho ni kitu ambacho hakiwezekani, so sikuhangaika kumtumia message, message niliyomtumia tu ni kumuuliza je uko sawa? Because najua [Vanessa] ni mtu mwenye moyo mdogo sana na akisingizwa anaumia sana. So kwasababu hakuwa nyumbani na alikuwa mbali mimi kitu cha kwanza nilichomuuliza ni ‘are you okay!’
Mimi amesema hofu kubwa ya Vanessa ilikuwa ni kwa mashabiki wake ambao wanaweza kuamini kuwa kweli anajihusisha na dawa hizo.
No comments: