Adam Juma ameacha kufanya video sababu Rama Dee amemuambia anazidiwa uwezo na Hanscana?
So Adam Juma ameamua kutangaza tena kuacha kufanya video za muziki baada ya Rama Dee kumwambia kuwa uwezo wake kwa sasa upo chini ukilinganisha na wa Hanscana?
Nimeandika kichwa cha habari kwa kuweka alama ya kuuliza kwasababu nitashangaa kama kweli kauli ya Rama Dee imemuumiza kiasi hicho Adam Juma hadi kuchukua tena uamuzi huo. Hii si mara ya kwanza Adam kutangaza kuacha kufanya video. Amewahi kusema hivyo miaka miwili iliyopita, lakini akatengua kauli yake kimya kimya na kuanza kufanya tena kwa jina la AJ.
“Mimi nimepumzika na sitaki kufuatilia mambo hayo ya muziki kila mtu ana misimamo yake na kwa sasa nataka niache kabisa mambo ya muziki nataka nifanye mambo yangu mengine ni ‘relax’ na kama kuna mtu anahisi mimi ni mjinga au mpumbavu ‘it’s fine,” Adam amenukuliwa akisema.
“Nimesikitika sana….sinto rudia kusema 🤐,” ameandika Rama Dee baada ya kusikia taarifa hiyo.
Naye rapper Godzilla ameandika: Too bad…kwa wingi wa kazi aliofanya Adam Juma…don’t disrespect him…Dhambi….ameshape hii industry ya video legend….hii mitandao isiwafanye muwe vichaa…thamini mchango wa mtu ….lame a$$&& niggas.”
Kama Adam ataamua kuachana na kufanya video kwasababu zake binafsi kama vile kubaki kufanya matangazo, documentary au filamu peke yake au kuona tu kuwa umri wake sasa hauendani na kazi hiyo, sitoshangaa. Nitashangaa kama ameacha kwasababu ya kauli ya Rama Dee. Nitashangaa kwasababu hakuna mtu ambaye hakosolewi kwenye kazi zake.
Tena, hakuna watu wanaopondwa kwa maneno ya kejeli kama wanamuziki. Hebu fikiria, yale maneno yote ambayo Diamond, Alikiba, Vanessa Mdee na wengine wanaambiwa kwenye mitandao ya kijamii, na mengi yakiwa ni matusi, wangekubali yawaumize nao waache kufanya muziki ingekuaje?
Nakubali kuwa Rama Dee hakuchagua njia nzuri ya kuufikisha ujumbe wake, ambao kwa wengi uliwakera, lakini haukupaswa kuwa na nguvu kubwa kiasi cha kumfanya AJ, ambaye kwangu ni kama P-Funk Majani wa video za muziki Bongo umuondoe kwenye kazi hiyo.
Ni kweli, vijana wapya kwenye video wana mbinu tofauti, lakini hatuwezi kuondoa ukweli kuwa Adam atabaki kuwa god father wa video za muziki Bongo na heshima hiyo haipaswi kuondolewa kwake. Karibu kila msanii aliyefanikiwa leo hii, amewahi kufanya video na Adam. Ni director wa kwanza Bongo kutengeneza video zenye hadhi ya kuchezwa kwenye vituo vya nje. Bado, mchango wake unahitajika mno hasa ukizingatia kuwa yeye ni msomi zaidi.
Kwahiyo, sina tatizo na Adam kuchukua uamuzi huo, ila nina tatizo na yeye kuamua hivyo kwasababu tu Rama Dee amemkosoa kwa maneno yaliyomuumiza!!

No comments: