Breaking News
recent

Sababu za Hispania kuteua Waziri anayeshughulika na mapenzi



Moja ya habari iliyomake headline kwenye vyombo vya habari vya kimataifa ni pamoja na hii iliyotokea Hispania ambapo Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mariano Rajoy amethibitisha uteuzi wa Edelmira Barreira kuwa Waziri wa mapenzi. Sababu zilizotajwa ni pamoja na hofu waliyonayo wanasiasa juu ya idadi ya watu inayoendelea kupungua tena kwa kasi ya kutisha.
Sababu nyingine iliyotajwa ni kuwa wanandoa wanashiriki mipango ya uzazi pia hawana nafasi na wapenzi wao, hii inatajwa ndio imesababisha idadi ya watoto wanaozaliwa kupungua sana. Aidha takwimu za hivi karibuni zimeitaja Hispania kama moja wapo ya mataifa yanayoongoza kwa kupungua kwa idadi ya watoto wanaozaliwa.
Waziri wa elimu  wa nchi hiyo hivi karibuni aliwasilisha ripoti yake kwa serikali na baraza la mawaziri akilalamika kwamba madarasa ya shule hayana idadi ya kutosha ya watoto na akaonya kwamba huenda ikaathiri Spain kiuchumi katika miaka ijayo.
Katika kushughulikia ishu hiyo kwa haraka Waziri mkuu wa taifa hilo Mariano Rajoy amemteua Edelmira Barreira kuwa waziri anayeshughulikia mapenzi. Kazi kubwa ya waziri huyo mpya ni kuja na mbinu za mikakati ya kuwahamasisha na kuuchochea umma kurudi vitandani na kusaidia kutengeneza watoto ili kuijaza tena Hispania.

No comments:


Powered by Blogger.