SPORTS EXTRA | WACHINA MBIONI KUINUNUA AC MILAN KWA DAU HILI
Biashara ya kuuzwa kwa klabu maarufu na kongwe mjini Milan nchini Italia AC Milan, inatarajiwa kukamilishwa mwezi ujao kwa kumshirikisha mmiliki wa sasa Silvio Berlusconi dhidi ya wawekezaji kutoka mashariki ya mbali (China).
Biashara hiyo inatajwa kufikia kiasi cha Euro milioni 740 sawa na dola za kimarekani milioni 818, sanjari na mkopo wa Euro milioni 220 ambao ulipaswa kulipwa tangu mwishoni mwa mwaka jana.
Silvio Berlusconi ambaye ni waziri mkuu wa zamani wa Italia, amekubali kufanya biashara ya kuiuza klabu hiyo kwa wafanyabiashara wanaomiliki makampuni ya Sino-Europe Sports Investment Management Changxing (SES), Haixa Capital na Yonghong Li.
Hii si mara ya kwanza kwa wafanyabiashara hao kutoka China kutaka kuinunua klabu ya AC Milan, mara ya kwanza walizungumza na Berlusconi na kufikia kiasi cha Euro milioni 320 ambazo zilikataliwa na baadae waliongeza Euro milioni 100 lakini bado biashara ilikua ngumu. Mazungumzo ya awali yalifanyika mwezi Agosti mwaka jana.
Hata hivyo tayari wafanyabiashara hao wameshalipa kiasi cha Euro milioni 200 na Machi 3 mwaka huu wanatarajia kumaliza kiasi kingine kilichosalia.
No comments: