JE WAJUA | Mwanajeshi wa zamani akataa kazi ya Trump
amependekezwa na Rais wa Marekani Donald
Trump kuwa mshauri wake wa masuala ya
usalama wa taifa amekataa kazi hiyo.
Robert Harward alitarajiwa na wengi kuchukua
wadhifa huo ulioachwa na Michael Flynn
aliyefutwa kazi na Bw Trump Jumatatu.
Afisa mmoja wa ikulu ya White House alisema
sababu ya Bw Harward kukataa nafasi hizo ni
kwamba ana majukumu mengi ya kifamilia na
kifedha.
Bw Flynn alimpotosha makamu wa rais Mike
Pence kuhusu mazungumzo yake na balozi wa
Urusi nchini Marekani ambayo aliyafanya kabla
yake kuteuliwa rasmi kuwa mashauri.
Pigo hilo kwa Bw Trump, la kukataliwa kwa
uteuzi wake na Harward, lilitokea saa chache
baada ya Bw Trump kupuuzilia mbali ripoti
kwamba utawala wake umekumbwa na
mtafaruku mkubwa.
Mshauri wa Donald Trump ajiuzulu
Familia ya Donald Trump: Wake na watoto
Watakaoumia na watakaofaidi chini ya
Trump Marekani
Alisisitiza kwamba utawala wake unafanya kazi
kama “mashine iliyoundwa vyema.”
Bw Harward aliambia shirika la habari la
Associated Press kwamba utawala wa Trump
ulikubali sana kuzingatia “mahitaji yangu, ya
kitaalamu na kibinafsi”.
“Ni suala la kibinafsi tu,” alisema Harward, 60,
ambaye kwa sasa anafanya kazi Abu Dhabi kama
afisa mkuu mtendaji wa kampuni inayofanyia
kazi jeshi la Marekani ya Lockheed Martin.
Alipoulizwa kuhusu taarifa kwamba alikuwa
amewasilisha ombi la kutaka aruhusiwe kuhama
na wafanyakazi wake binafsi serikalini, Bw
Harward alisema: “Nafikiri rais ndiye anayefaa
kuzungumzia hilo.”
Watu wawili wanaopigiwa upatu sana kupewa
wadhifa huo ni Jenerali mstaafu David Petraeus
na kaimu mshauri mkuu wa masuala ya usalama
wa taifa Keith Kellogg.
Bw Kellogg, ambaye ni jenerali mstaafu wenye
nyota tatu, aliteuliwa kuhudumu kama kaimu
baada ya Bw Flynn kung’atuka.
Ana miaka 72 na amehudumu kwa muda mrefu
jeshini, ambapo alipigana vita Vietnam na Iraq
kabla ya kustaafu 2003 na kuwa mshauri wa
masuala ya usalama wa kampuni ya programu
za kompyuta ya Oracle Corp.
Obama: Sitanyamaza utawala wa Trump
Kijana aliyepanga kumuua Trump afungwa
Mbona Air Force One ni ghali mno?
Bw Petraeus, ni jenerali wa zamani mwenye
nyota nne, ambaye alistaafu kama mkuu wa CIA
mwaka 2012 baada ya kubainika kwamba
alikabidhi nyaraka zenye siri kuu kwa mwandishi
aliyekuwa akiandika kitabu kuhusu maisha yake,
ambaye alikuwa ameingia kwenye uhusiano nje
ya ndoa naye.
Bado anatumikia adhabu ya kuwa chini ya
uangalizi kwa miaka miwili kwa kosa la
kutomakinika akiwa na nyaraka za siri.
Atahitajika kumfahamisha afisa wa jela
anayemfuatilia iwapo atahitaji kuhamia
Washington DC.
No comments: