Breaking News
recent

ENEWZ MAMTONI | RAIS WA TUZO ZA GRAMMY AFUNGUKA SAKATA LA UBAGUZI JUU YA GRAMMY




Baada ya kuwa na malalamiko kuhusu kipengele cha “Album of the year” kwenye tuzo za Grammy kuwa kwamba kinabagua watu kwa rangi zao, Raisi wa Grammy ameamua kufunguka juu ya hilo.
Neil Portnow, Raisi wa tuzo za Grammy ameamua kufunguka juu ya sakata ambalo bado linaendelea midomoni mwa watu pamoja na kwenye mitandao ya kijamii kwamba tuzo za Grammy hutolewa kwa upendeleo, Portnow amefunguka kwa kusema kwamba “anaamini kwamba kura zinazopigwa kwenye tuzo hizo ziko fair kabisa kwa watu wote bila kubagua”.
Ishu hiyo imeanza kuwa kubwa baada ya Adele kunyakua tuzo ya Album of the Year ambayo alikuwa anachuana na Beyonce, sasa mashabiki wameamua kuja juu pamoja na kuleta listi nzima pindi inapofika swala la wamarekani weusi kuchukua tuzo ya Album of The Year huwa wanahujumiwa, mpaka sasa unaambiwa kuna wanawake watatu weusi ambao wamechukua tuzo hiyo ni Natalie Cole (1992) ‌• Whitney Houston (1994) ‌• Lauryn Hill (1999).
Hata hivyo Portnow amefunguka kwa kusema kwamba ndio mana Chance the rapper ametajwa kama Best new artist of the year kuonyesha kwamba hakuna tofauti ya kirangi juu ya tuzo hizo.

No comments:


Powered by Blogger.