ENEWZ AFRICA | Diamond amefanya vitu vingi vikubwa hadi sasa vinaanza kuoneka vya kawaida? Mfano ni
Kuna kipindi Javier Mascherano, mwanasoka wa Kiargentina alinukuliwa akisema haya juu ya Lionel Messi ‘Kinachomsumbua Messi kwa sasa ni uwezo wake mkubwa na mambo makubwa ambayo amefanya mpaka yameanza kuonekana ni mambo ya kawaida.’
Diamond ameachia ngoma yake na Ne-Yo iitwayo Marry Me. Yeye mwenyewe anasema kwake ni ndoto iliyotimia. Ukiwatoa wale mashabiki wake wakubwa, watu hawaoneshi kujali wa la kushtuka na wala kuonesha kukubali kwa kiwango ambacho naamini wanatakiwa waipokee ngoma hii naamini kufanya wimbo na Ne-Yo sio kitu kidogo.
Lakini mwisho wa siku nakuja kugundua pengine sio kosa la mashabiki na wadau kutoona kama hiki ni kitu kikubwa kwa kiwango hicho ni kosa lake mwenyewe Diamond! Ndiyo kosa lake amefanya vitu vingi vikubwa mpaka inafikia kipindi vinaaanza kuonekana sio story tena.
Hakuna kipya ambacho unaweza ukasema sasa ambacho Diamond hajakisikia iwe kwa kumsifia au kumtukana lakini hii ni kubwa sana kaka mkubwa kwa Leo inaweza isionekane hivyo lakini siku moja itabaki kuwa ni moja Kati ya alama kubwa kuwahi kuziweka kwako wewe na muziki wa Bongo Flava kwa ujumla.
Haijalishi unampenda au humpendi Diamond hayo ni maamuzi ya moyo wako na wala haikatazwi,lakini lazima tukubali kuwa Platinumz sasa ni habari nyingine. Kuwa na kipaji ni jambo moja lakini kuweza kuishi katika lile ulilojaaliwa na mwenyezi Mungu inahitajika akili, maarifa na juhudi za kiwango cha juu sana.
Keep this thing alive Platnumz,inawezekana isionekane sasa ila siku moja kila mmoja atakiri kuWa angalau ulichangia kuufukisha mUziki pale utakapokuwepo na alama yako itabaki milele hata baada ya wewe kuondoka duniani. Na usishangae hata collabo zako ulizosema na Rihanna na Rick Ross zisije kuwashtua watu kama ilivyotokea kwa hii ya Ne-Yo, lakini tambua kuwa unatengeneza historia ambayo haitofutika na thamani yake itakuwa kubwa miaka ya mbele kama uwavyo mvinyo.
No comments: