Breaking News
recent

MIMI MARS AFUNGUKA KUHUSU MDEE MUSIC KUSAINI WASANII WAPYA


Msanii wa Bongo Fleva toka Mdee Music, Mimi Mars amesema kwa sasa lebo hiyo haina mpango wa kumsaini msanii mpya ingawa kuna ambao wanawaangalia.
-
Akizungumza na Mtangazaji Lil Ommy katika Podcast ya kwanza ya Audiomack Africa, #SwahiliRadio Mimi Mars amesema kwa sasa wanatazama wasanii wapya ambao wanajaribu kutoka kupitia mitandao ya kijamii.
-
"Wapo wengi tunawaangalia licha ya Vee kutokuwepo lakini yupo kwenye mfumo, kuna wasanii tunawaangalia wale ambao wanakua kwa sababu sasa hivi all upcoming artist wanajiweza, wanajua nini cha kufanya," amesema.
-
"So tunawatafuta wale ambao tunaona wanaimba tu kwenye social media tu, wanaimba cover za nyimbo za watu. Ndio tunafanya, lakini kusema tutasaini msanii mpya mwaka huu au mwakani, hilo hapana, sio kweli," amesema Mimi Mars.
-
Ikumbukwe Lil Ommy amekuwa Mtangazaji wa kwanza Afrika kuchaguliwa na Audiomack kufanya Podcast ya kwanza ya #AudiomackAfrica, Swahili Radio ambayo itasikika nchi 54 za Afrika na dunia nzima kupitia Audiomack App, Website yao pamoja na mitandao yake ya kijamii.
 

No comments:


Powered by Blogger.