NYIMBO ZANGU ZOTE HUWA NI HIT - MARIOO
Msanii wa Bongo Fleva, Marioo amesema yeye ni mwimbaji ambaye amefanikiwa kutoa hit songs nyingi sana kwenye muziki huo kwa kipindi kifupi, hivyo anastahili kuwa Mfalme wa kizazi cha sasa.-
Marioo ameeleza hayo akiongea na Lil Ommy katika Podcast ya kwanza ya Audiomack Africa, #SwahiliRadio ambapo amesema nyimbo zake Mama Amina, Chibonge, Inatosha na Dar Kugumu zilifanya vizuri kiasi cha kuzima mitaa.
-
"Nyimbo zangu zote ni hit sema zinatofautiana ukubwa, kupata wimbo mkubwa kama Mama Amina unaweza kupata mmoja kwa miaka hata mitano, lakini mimi nazipiga nyingi. Kuna Mama Amina, Chibonge, Dar Kugumu, hizo zote ni nyimbo za Taifa, nikizungumzia nyimbo za Taifa, ni nyimbo ambazo huwa zinazima mitaa yote," amesema.
-
"Kama Mama Amina, Chibonge, Inatosha na Dar Kugumu zilivuma sana, na lazima ziwe namba moja kwenye chati zote za redio Tanzania, so nimefanikiwa kuzipiga hizo nyingi sana kitu ambacho si cha kawaida," amesema Marioo.
-
Ameendelea kwa kusema,"Wasanii wengi wanafanikiwa kupiga hiyo moja kisha anatoa hit za kawaida, lakini mimi napiga, halafu natoa hit ya kawaida kama For You halafu nashindilia nyingine tena".
-
Utakumbuka Lil Ommy amekuwa Mtangazaji wa kwanza Afrika kuchaguliwa na Audiomack kufanya Podcast ya kwanza ya #AudiomackAfrica, Swahili Radio ambayo itasikika nchi 54 za Afrika na dunia nzima kupitia Audiomack App, Website yao pamoja na mitandao yake ya kijamii.
No comments: