Breaking News
recent

G Nako amtolea uvivu Tox Star

Baada ya msanii Tox Star kudai kuwa Belle 9 na G Nako wameiba kiitikio cha wimbo wake na kwenda kukitumia katika wimbo wao ‘Ma-Ole’, G Nako amesema si kweli na akiwa studio huwa hamuwazi mtu yeyote.


G Nako
G Nako ameimbia EATV kuwa mara nyingi anapofanya kazi zake studio huwa yupo katika zone yake mwenyewe, kwenye hisia zake za tofauti, kwa hiyo ni ngumu kutoa kitu kinachofanana na mwingine.
“Kinaweza kuwa kimefanana kwa namna ambayo ni melody za kimuziki lakini hakiwezi kufanana kwa asilimia 100, kwa sababu mara nyingi unaweza kukuta code za muziki zinaingiliana, hivyo ni vitu ambavyo huwa vinatokea lakini sijawahi kufanya kitu nikacompare na msanii mwingine, pia sijawahi kufanya kitu kwa sababu nimesikia kwa mtu mwingine,” amesema G Nako.

No comments:


Powered by Blogger.