THOMAS TUCHEL MBIONI KUMRITHI ARSENE WENGER
Klabu ya Arsenal imeripotiwa kuwa katika mipango ya kumuajiri meneja wa klabu ya Borussia, Dortmund Thomas Tuchel, kama mbadala wa Mkongwe Arsene Wenger.
Mipango hiyo ya Arsenal imefichuliwa na jarida la michezo la Ujerumani la Bild, ambapo inadaiwa viongozi wa The Gunners wamemfuatilia Tuchel na kubaini anaweza kurithi mikoba ya Arsene Wenger, ambaye kwa sasa amekalia kaa la moto.
Tuchel mwenye umri wa miaka 43, aliajiriwa Westfalenstadion mwaka 2015 akitokea kwenye klabu ya Mainz, na kwa kipindi hiki amekiwezesha kikosi chake kupambana na kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ya Ujerumani (Bundesliga).
Tuchel alikabidhiwa kijiti cha kuwa mkuu wa benchi la ufundi klabuni hapo, baada ya kuondoka kwa Jurgen Klopp mwishoni mwa msimu wa 2014-15.
Uongozi wa Arsenal upo kwenye mipango ya kumsaka meneja mpya, kufuatia mkataba wa Arsene Wenger kutarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu, japo kuna tetesi zinazodai huenda mzee huyo wa kifaransa akasaini mkataba wa mwaka mmoja.
No comments: