Breaking News
recent

Nini kinaendelea kwa Enika na Grace Matata?

Katika dunia yenye utitiri wa watu inawezekana mtu kuwa na kipaji katika eneo fulani sio ishu tena. Kuna vipaji lukuki duniani na pengine pamoja kua kipaji maridhawa haswaa unaweza usipate nafasi kama ambavyo ilistahili iwe kulingana na ubora wa kipaji chako.

Wakati ukiwa ni mwezi ambao dunia inasherehekea uwepo wa kiumbe adhimu na chenye mvuto wa pekee mwanamke na pengine kila mmoja akijaribu kuonyesha ukubwa, nafasi na mchango wa kipekee wa mwanamke katika maeneo mbalimbali,pengine akili na moyo wangu upo nyuma ya wakati.
Nasema hivyo pamoja na kuwa na wanawake wenye vipaji katika muziki wetu eti mimi akili yangu imegota nabaki kukumbuka watu ambao hatuwasikii tena kwenye media angalau hata midomoni mwa watu pamoja na akili yangu kuamini kuwa vipaji vyao sio vya nchi hii kama wasemavyo watoto wa kwetu kule uswahilini.
Ebu subiri,unakumbuka ile ngoma inaitwa Baridi kama hii,yenye sauti tamu na mashairi fulani ya kusisimua au labda nikukumbushe moja kati ya kolabo kali kuwahi kuzisikia kwenye kiwanda cha Bongo Flava rudi nyumbani achana na ile sauti tamu ya kiume kumbuka ile ya kike yenye kulalama mule ndani,kama unapenda Hip hop basi kumbuka ile chorus ya N2N soldiers Hawatuwezi.
Achana na huyo,kuna nyimbo fulani inaitwa Free Soul,moja kati ya nyimbo zenye mashairi makali sana yanayotoka kwenye kinywa ambacho mwenyezi Mungu alikipa sauti yenye ladha ya kipekee sana,na naamini sitaonekana mshamba nikisema ya kumtoa nyoka pangoni,na song zingine kali kutoka kwenye kinywa cha mwanadada huyo hakika ukisikiliza halafu ukasema hana kipaji ni bora uendelee na mbishe nyingine.
Pengine nimezunguka sana,labda nilikuwa nataka nijenge picha na kurudisha kumbukumbu juu ya ubora wa vipaji vya mabinti hawa yani Grace Matata na Enika,sijui wako wapi? Sijui bado wanafanya muziki? Au ndo wapo busy na mishe zingine za kutafuta maisha baada ya kuona muziki haurudishi kile ambacho walikitegemea kutoka huko?
Kwa vyovyote vile,Enika na Grace Matata ni vipaji haswa,pengine kama nilivyosema mwanzo kipaji katika zama hizi sio kitu pekee kitachomfanya msanii afike sehemu yenye mafanikio kuna mambo mengi inabidi yafanyike mpaka mtu aonyeshe uwezo wake alojaaaliwa ma maulana. Naamini kuna kitu hakijafanyika kwa wadada hawa na ndiyo sababu pamoja na ubora wao hawasikiki kama inavyotakiwa.
Imani yangu kama sio tu kwa wao kuwa wameamua kutulia na kutoupa muziki kipaumbele,basi hawa ni moja kati ya vipaji maridhawa vya kike kutokea nchini. Wakati tukifikiria namna ya kuongeza namba ya wasanii wa kike kwenye ramani ya muziki,hatutojuta kama tutaamua kuwekeza nguvu,mali na akili zetu kufanya hivi vipaji visibaki kua story tu.
Na Eliezer Gibson

Instagram gibson_elly

No comments:


Powered by Blogger.