Breaking News
recent

HATIMAE NDOA YA LULU, DJ MAJIZO YANUKIA, LULU ANYOOSHA MAELEZO

Msanii mahiri wa filamu Bongo, Elizabeth Michael aka Lulu baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, ameibuka na kuweka wazi kwamba yupo mbioni kukamilisha maandalizi ya ndoa yake na mmiliki wa Redio, Francis Shiza ‘Dj Majizo’.
Katika mahojiano na Gazeti la Mtanzania wiki hii, Lulu, ambaye hivi karibuni alidaiwa kuachana na mpenzi wake huyo wa muda mrefu, alidai  kwamba taarifa hizo hazikumuumiza, ndiyo maana aliamua kuwa kimya, huku akiendelea na mipango yake ya ndoa na mpenzi wake huyo.
“Siku zinakaribia na karibu tarehe ya ndoa yangu itatangazwa kwa uwezo wa Mungu, hapo ndipo waliotamani tuachane wataziba midomo, maana natarajiwa kuwa mke halali hivi karibuni,’’ alisema Lulu.
Lulu aliongeza kwamba, atakapoolewa amepanga kuwa mke mwema kama anavyoishi sasa kwenye hatua za uchumba.

No comments:


Powered by Blogger.