Breaking News
recent

Namtamani Lulu na Wema Sepetu – Msami

Msanii wa muziki Msami Baby ameweka wazi hisia za moyo wake kwa kuwataja mastaa watatu wa bongo movie ambao anatamani kutoka nao kimapenzi.
Muimbaji huyo amemtaja Wema Sepetu, Elizabeth Michael (Lulu) pamoja na Jokate Mwegelo kuwa ni wanawake anaowatamani zaidi ndani ya bongo movie.
“Katika mastaa wa bongo ambao ninawapenda sana na ninatamani ningewapata ni pamoja na Jokate Kidoti, Lulu na Wema Sepetu, uzuri wa hawa wadada unanifanya niwapende sana” Msami alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.
Kwa upande mwingine msanii huyo amesema yeye umri kwake siyo kigezo kikubwa kwakuwa ameshawahi kutoka na mwanamke aliyemzidi umri na wakaishi vizuri bila ya kuwa migogoro ya aina yeyote ile.

No comments:


Powered by Blogger.