Breaking News
recent

HIVI NDIVYO AMBAVYO SKENDO YA MADAWA IMEMNUFAISHA WEMA SEPETU


Wiki chache zilizopita akili na macho ya watanzania woengi vilikuwa katika sakata zima la kupambana na madawa ya kulevya, sakata ambalo lilipewa kupaumbele na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda.
Sakata ambalo liliwagusa watu wengi maarufu akiwemo mwanadada Wema Sepetu. na kusababisha mrembo huyo kukaa rumande, na kusota mahakamani kwa  siku kadhaa.
Wengi walifahamu kwamba sakata hilo limemgharimu sana Wema Sepetu ikiwa ni katika kuharibu brand yake na vitu kama hivyo. Unachotakiwa kukifahamu ni kwamba kuna faida ambayo Wema Sepetu ameipata kutokana na sakata hilo.
Ikumbukwe kwambasakata hilo lilianza siku mbili baada ya Wema Sepetu kuzindua application yake mpya. Application ambayo inawawezesha mashabiki zake kufahamu habari zake nyingi na kwa haraka zaidi.
Meneja wa Wema SepetuMartin Kadinda ameiambia DJ PAUL24 kwamba ni pesa nyingi sana ambazo application ya Wema Sepetu iliingiza wakati wa sakata la madawa ya kulevya kwasababu kila mmoja alikuwa anataka kujua habari za Wema na hakuna sehemu nyingine zilipoweza kupatikana ispokuwa kwenye application pekee.

No comments:


Powered by Blogger.