Breaking News
recent

SPORTS EXTRA | Picha,Rafiki wa karibu wa Cristiano Ronaldo aliyehukumiwa miaka miwili jela, sababu….



Mshkaji wa karibu wa mwanasoka maarufu duniani Cristiano Ronaldo ahukumiwa kifungo cha miaka miwili jela, Badr Hari ni bingwa wa mchezo wa kickboxer mwenye umri wa miaka 32, amehukumiwa kwenda jela miaka miwili baada ya kupatikana na hatia ya shambulizi.
Badr Hari na raia wa Morocco aliwahi kuzushiwa kuwa kwenye mahusiano ya jinsia moja dhidi ya mwanasoka bora duniani Cristiano Ronaldo mchezaji wa Real Madrid baada ya picha kusamba akiwa amembeba.
Hukumu dhidi ya Badr Hari imetolewa nchini Uholanzi, hivyo atalazimika kutoka kwao Morocco kwenda jijini Amsterdam kutumikia kifungo chake.
Hukumu inasema hakutakuwa na rufaa hadi atakapotumikia kifungo kwa miezi sita kwanza, baada ya hapo ndiyo mwanasheria wake anaweza kuifikisha rufaa sehemu husika.
Tetesi zinasema Badr Hari anaweza kuamua kutokwenda nchini humo tena ili asikamatwe na kupelekwa gerezani.

No comments:


Powered by Blogger.