Breaking News
recent

ENEWZ AFRICA | Darassa akerwa na suala la warembo wale wale kujirudia kwenye video za Kibongo

Kuna kasumba ya kuigana na kufanana kwa vitu inaendelea kwenye video za muziki za Kibongo. Tumewahi kuandika Makala kuhusu video nyingi kuwa na moshi na baruti.




Jumatatu hii Babutale alizungumzia kuhusu waongozaji kutumia location na magari yale yale kwenye video wanazofanya. Lakini pia kubwa lililopo sasa ni warembo wanaotumika kwenye video kuwa wale wale? Kwanini?
Kwenye teaser ya mahojiano ya kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha Salama Jabir kitakachoruka Alhamis hii kupitia EATV, hitmaker wa Muziki, Darassa amezungumzia suala hilo.


“Inanipaga tabu, na ukiangalia watu wengi ambao naanza kushoot nao, baada ya kushoot nao wataonekana kwenye video nyingi,” anasema rapper huyo.
“Sababu nataka niwatengeneze iwe na maana ya wao kuwa kwenye video, hakukuwa na sababu ilibidi tu uwepo pale. Kuwe na maana ya kuwepo pale, so huwa natengeneza hadhi yake na heshima yake na parts ambazo anaenda kuzifanya zinaconvince watu wengi baadaye kumwalika kwenye video zake,” amesisitiza rapper huyo.
Miongoni mwa video vixen wanaonekana zaidi kwa sasa ni Gigy Money na Amber Lulu

No comments:


Powered by Blogger.