Breaking News
recent

ENEWZ AFRICA | Aika Afunguka Jinsi SAUTI SOL Walivyozingua Kufanya Ngoma Ya Lini


Unaweza kudhani kwamba kwa ukubwa wa Navy Kenzo na muziki wao kwasasa Barani Africa hakuna mtu ambae anaweza kuzingua kufanya nao collabo, hakuna ukweli juu ya hilo. Unachotakiwa kufahamu ni kwamba ugumu na changamoto za kazi bado ziko pale pale.
Amelithibitisha hilo mwanadada Aika wa Navy Kenzo baada ya kutusanua ni vipi kundi la muziki nchini Kenya Sauti Sol lilivyo zingua kufanya ngoma ya Lini ambayo ameshirikishwa Alikiba.
Aika amefunguka kuwa kabla ya ngoma hiyo hawajampelekea Alikiba walipewa kwanza Sauti Sol ili waweze kufanya kitu, lakini matokeo yake ukimya ulikuwa mwingi na kuonyesha dhahiri kuwa hawakuwa tayari kushiriki katika ngoma hiyo.
Na hivyo baadaye ndipo Navy Kenzo walipoamua kuupelekea uongozi wa Alikiba ngoma hiyo na wakaipenda mwisho wa siku ikawa kituu.


No comments:


Powered by Blogger.