Breaking News
recent

UDAKU | Picha: Rapper wa Malawi Tay Grin, Diamond na Mohombi washoot video SA

Tuzo za MTV MAMA huwakutanisha wasanii wengi wa Afrika kwa wakati mmoja. Si kila anayehudhuria huwa ametajwa kuwania tuzo, bali wengine huenda kwaajili ya kutafuta connection.


                                     Rapper wa Malawi, Tay Grin akiwa na Diamond

Na wengine hutumia fursa hiyo kwenda kufanya video na wasanii waliowashirikisha ili kupunguza gharama za kuwasafirisha kuwapeleka SA kwaajili hiyo. Miongoni mwa watu waliotumia fursa hiyo ni rapper wa Malawi, Tay Grin aliyewahi kuweka wazi nia yake ya kutaka kufanya kazi na Diamond.


Diamond akiwa na Tay Grin mwenye fulana nyeusi, msanii wa Sweden mwenye asili ya DRC, Mohombi na wengine

Na sasa huenda hilo limekamilika baada ya kuungana na muimbaji huyo wa ‘Salome’ jijini Johannesburg kufanya video ya wimbo unaonekana amemshirikisha Diamond pamoja na msanii wa Sweden, Mohombi.
“We out here with the boy @diamondplatnumz video shoot,” ameandika Tay Grin kwenye picha hiyo ya juu aliyoiweka Instagram. “It’s fire trust! With @mohombimusic ( I wanna boom bang bang with your body ðŸ”Š) @iamlumino @chronicles_of_karim_cazal colin the “boss” it’s all love out here! Great things in the pipeline.”
Naye Mohombi aliweka picha akiwa na Diamond kwenye mtandao huo na kuandika: Big Things Coming !!!! #AfricaUnite with my bro @diamondplatnumz.”

Mohombi ambaye alikuja Tanzania kweye Fiesta mwaka 2014, anafamika zaidi kwa hit zake zikiwemo Bumpy Ride, Coconut Tree aliomshirikisha Nicole Scherzinger na Miss Me aliowashirikisha Nelly na Snoop Dogg.


No comments:


Powered by Blogger.