Breaking News
recent

JE WAJUA | Bumbuli ina miti hii ambayo Mizizi yake inaota kwenda Juu kama Ukuta..



Vipo vitu ambavyo ukivisikia unakua na maswali mengi sana kichwani,katika vitu ambavyo nimekutana navyo ni pamoja na hii ya Mizizi kuota kuelekea juu kama ukuta sio chini tena kama ambavyo tumezoea kwa mimea mingine.
Mti huu unaitwa Entandrophragma Excelsum unapatikana kwenye Msitu wa Mazumbaiuliopo Bumbuli kwenye wilaya ya Lushoto kwenye mkoa wa Tanga na kizuri zaidi Msitu huu umehifadhiwa na Serikali chini ya chuo kikuu cha Sokoine kwa ajili ya watu kwenda kujifunza.
Msitu huu wa Mazumbai nimewambiwa unasifa nyingi sana za kipekee,kwanza ni kati ya misitu michache ambayo haijaathiriwa na shughuli za kibinadamu na hii ni kutokana na ulinzi uliopo hapo pia msitu huu una aina nyingi za mimea kuliko aina za mimea inayopatikana Ulaya Magharibi.

Waziri wa Nchi Ofisi Ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano Na Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli Mh.January Makamba ni miongoni mwa Wageni waliopata nafasi ya kutembelea msitu huu.


KWA HABARI MBALIMBALI ZA ULIMWENGUNI KOTE USIACHE KUTEMBELEA BLOG HII KUFAHAMU MENGI ZAIDI..



No comments:


Powered by Blogger.