Breaking News
recent

UDAKU | Huyu ndiye mchina wa Ommy Dimpoz ambaye alidai anatoka naye kimapenzi?


Mkali wa wimbo ‘Kajiandae’ Ommy Dimpoz wiki kadhaa zilizopita alidai ukifika wakati atamweka wazi mpenzi wake ambaye ni mchina.


Ommy Dimpoz akiwa na mrembo wa kichina
Muimbaji huyo ambaye amekuwa msiri kwenye suala la mahusiano yake ya mapenzi, alithitisha kupitia EATV kwamba kwa sasa yupo kwenye mahusiano na raia wa China, ambaye watu wengi hawamjui.
Jumanne hii muimbaji huyo ameanika picha ya mrembo wa kichina Instagram na kuweka ’emoji’ za mapenzi.
Hata hivyo muimbaji huyo hakutaka kufungua mjadala kwenye picha ile kwa kuamua kufunga uwanja wa comment ili watu wasiweze kuzungumza wala kujadili katika picha hiyo. Lakini ukweli ni kwamba picha ile inazungumza mambo mengi kwa kila anayeiangalia.


No comments:


Powered by Blogger.